SOMA KWANINI KUNDI LA ORIJINO KOMEDY LIMEMWAGWA CHINI, MANAGER AONGEA

 

ORIJINOKOMEDI

waigizaji wa kipindi cha orijino Komedi kutoka kushoto ni Joti, Wakuvanga, Mpoki, Masanja mkandamizaji na Maclegan.
KUNDI maarufu la vichekesho ambalo kwa sasa ni kama halipo, limepata pigo kubwa baada ya aliyekuwa meneja wao, mtangazaji nyota wa zamani wa televisheni, Christina Mosha maarufu kama Seven, kuwamwaga na hivyo kuachana nao. 
 
Akizungumza na gazeti juzikati, Seven alisema ameachana nao baada ya mkataba wake wa sasa kumzuia kufanya kazi na watu wengine zaidi ya walio chini ya mwajiri wake mpya. 
“Hivi sasa niko na Sony, wao wananizuia kufanya kazi na wasanii ambao hawako nao, hivyo baada ya mkataba wangu na wao kumalizika, nimeamua kuachana nao.
seven
Aliyekuwa meneja wa kundi la Ze Comedi, mtangazaji nyota wa zamani wa televisheni, Christina Mosha maarufu kama Seven akifafanua jambo.

 

 Mimi ni mwakilishi wa Sony barani Afrika, ninashughulika na wasanii toka nchi tofauti za Afrika, kama Senegal, Kenya na kwingineko kasoro Afrika Kusini,” alisema.
Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :NGG UMOJA RADIO

Tupe maoni yako hapo Chini..!!