Tamasha la Diamond Platnum lililofanyika jana ukumbi wa maonyesho Sindelfingen Stuttgart laingia kitimtim baada ya mashabiki kufanya fujo za hali ya juu ikiwa ni pamoja na kurusha chupa , iliopeleka watu kuumia , hali ya ya sintofahamu imetokea baada ya mashabiki kumsubiria Diamond apande stejini kwa mda mrefu lakini kinyume na matarajio yao na kupelekea Mwanamziki huyo kufika ukumbini saa kumi alfajini ,
kitendo hicho kilipelekea mashabiki wakasilike na kuanza kufanya fujo za hali ya juu, na kupelekea polisi wafike eneo hilo kwa haraka ili kutuliza ghasia na kuweza kumuokoa mwanamziki huyo , pia magari sba aya ambulance yalifikwa kwa haraka kusaidia majeruhi zaidi ya kumi na nane waliokuwa wameumia ikiwa pamoja na ma DJ wa tamasha hilo ,
pia upotevu wa vitu mbalimbali kama Computer na vitu vingi katika fujo hizo , ilipelekea mashabiki kuwalalamikia waandaaji wa tamasha hilo kwa kitendo walichokifanya , na wengi mpaka sasa wakidai japo warudishiwe pesa zao kwani si haki watu kusafiri kutoka nchimbalimbali kwa ajiri ya kumsapoti msanii wao harafu washindwe kumuona na hata kupaform Aliongea shabiki wa Diamond. Mpaka sasa haijajulikana waandaaji wa TAMASHA HILO WAKO WAPI KWANI HAKUNA HATA MMOJA ALIEPATIKANA:
Daimond akiwa Germany
Diamond nae hakukaa kimya alikuwa na haya ya kusema
kiukweli nimesikitishwa sana na uandaaji wa kampuni hii ya BRITTS EVENTS iliyoandaa show ya Stuttgart Germany… kinachoniuma na kunisikitisha zaidi ni jins watu walivyoamua kujitolea kuja kutusupport vijana wao kwa wingi, halaf mwisho wa siku promoter anatupeleka wasanii kwenye show saa kumi alfajiri… najua ni kiasi gani mmeumia na kuwa disappointed… lakini naomba mtambue kuwa halikuwa ni kosa langu, coz mimi ni mgeni tu, na nafata maelekezo ya promoter…hivyo nisingeweza kujiamulia kuja muda ninaoutaka mimi…
Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more
CREDIT : HERE
Tupe maoni yako hapo Chini..!!