Hokelai Mganga during one of the filming sessions.
Mwaka 2004, Lupita Nyong’o alipokuwa anakuja Zanzibar International Film Festival (ZIFF)nadhani hakuna aliyekuwa anajua malengo yake ya baadae. Ila nafsi yake ilikuwa inaona mbali sana kwenye mafanikio. Mwaka jana ameweza kuigiza filamu bora kwa sasa “12 Years a Slave”.
Changamoto kubwa zinazowakabili wasanii wa Tanzania na hata na WALIMU wa hii tasnia ni kushindwa kujiendeleza kielimu. WALIMU wameng’ang’ania uwezo walio nao kama vile ndio mwisho wa kila kitu. Kwa mfano tunatamasha la ZIFF, wenyewe wanahangaika kuandaa mafunzo kila mwaka, tena kwa gharama kubwa. Kwa mwaka juzi nilikuwa coordinator wa workshop ya HD chini ya Barry Braverman na workshop ya Editing chini ya Nicolas Stampe yani unaona aibu, wanafunzi/wasanii walijitokeza wachache mnoo.
Mpaka unabembeleza kwa wengine lakini unawapata wasanii wale wale wanaonyesha jitiada Peter Mbwago, Makoti Wahapahapa , Richard Magumba , Rutakirwa Kasiga , Mshindo Ally, David Nelson Shija na mwalimu wangu naye utamkuta yumo Vicensia Shule. Waliobaki wote wanatoka nje ya Tanzania, masikini Prof. Martin Mhando anajitaidi kutafuta wataalamu bora lakini Watanzania masikio wameziba. Mwaka 2012, workshop ya screen writer chini ya Maisha Film Lab kwa ajiri ya Watanzania, waliomba ni Watanzania WATATU TU. Kuna kikao kilifanyika cha kujadiliana maswala ya Filamu kwa East Africa, walikuwemo kutoa michango wote walikuwa kutoka nje na Wanzania wawili tu Vicensia Shule na Issa Mbura na mwenyekiti alikuwa prof. Martin Mhando.
Lupita attends the 71st Annual Golden Globe Awards.
Waliobakia wote kutoka Kenya (Walileta mpaka na Waziri na watu wa Bodi ya Filamu ya kwao), Uganda, Rwanda, Burundi. Ili tasnia ikuwe lazima WALIMU na WASANII wote wajifunze kila kukicha vitu vinakuwa vipya, lakini bila hivyo tutabakia na wafanyakazi wengi wa BANK ambao wamesomea FILAMU na SANAA. Lupita yeye aliamua kusoma zaidi masters pale Yale School of Drama, na kwa sasa anatengeneza mafanikio kibao. Na mafaniko unatakiwa kuwekeza, kwenye mafunzo zaidi pia.
Na kingine hatuna nafasi kubwa ambayo uanaweza kukutana na wasanii wakubwa Duniani kwa East Africa kama ZIFF. Ndio link kubwa ya msanii kukutana na msanii ambaye amekuzidi, anakusaidia kwa namna moja au nyengine. Tutabakia kuwa WAKOSOAJI wa movie zetu kila kukicha lakini hatua ya kutengeneza zilizo bora hakuna, huku fulsa wanawahi watu kutoka nje.
Usisahau kulike and share pia unatupata facebook . swahili movies .com
pia follow us instagram swahilimovies