Update on Garisa :Wasomali walalama kufungwa kwa Hawala Kenya

 

150406100153_kenya_soldier_512x288_getty_nocredit

Jamii ya wasomali nchini Kenya wamelalamikia vikali hatua ya serikali nchini humo kufunga mashirika kumi na tatu ya ubadilishaji wa sarafu za kigeni na usafirishaji pesa maarufu kama Hawala.

Malalamishi yao ni kuwa hatua hiyo itasababisha matatizo makubwa kwa wasomali ambao daima wanategemea njia hiyo, kuwatumia jamaa zao fedha kutoka mataifa ya kigeni.

Hatua hiyo imefanyika baada ya shambulio la Al-Shaabab katika Chuo kikuu mjini Garrisa juma lililopita.

Serikali ya Uhuru Kenyatta inasema kuwa ni mojawepo ya njia ya kuzuia al-Shabaab kupata fedha ili kupanga na kutekeleza mashambulio zaidi.

Hali ya hatari ya kutotembea nje usiku pia imewekwa katika majimbo yaliyo na wasomali wengi kazkazini mashariki mwa Kenya.

Akaunti za Benki za watu themanini na sita zinazodhaniwa kufadhili ugaidi pia zimesitisha.

150406123126_kenya_640x360_bbc_nocredit

NB:BBC Dira TV: Baadhi ya viongozi wa Kaskazini Mashariki mwa Kenya wanataka kambi za wakimbizi kufungwa kwa vile wanahisi zinatumika na baadhi ya watu kupanga mashambulio ya kigaidi. UNHCR inasema hakuna ushahidi wa jambo hilo. Nini maoni yako?
Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :   BBC NEWS

Tupe maoni yako hapo Chini..!!