Uwoga wetu na kutojiamini kunachelewesha muziki wetu kuwa mkubwa duniani – Diamond

Uwoga wetu na kutojiamini kunachelewesha muziki wetu kuwa mkubwa duniani – Diamond
By Salum Kaorata |

Kupitia wimbo wa ‘Hallelujah’ umekufunza nini? Hilo ndio swali ambalo Diamond anawauliza mashabiki wake kwa sasa.

Kwa Diamond ambaye ndio msanii husika wa wimbo huo umemfundisha jambo moja kubwa ambalo ni uwoga wa wasanii wetu wa Bongo wa kushindwa kujiamini ndio unacheleweshea muziki wetu kutoboa zaidi duniani. Muimbaji huyo wa WCB amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram, Jumamosi hii.

Kupitia mtandao huo, Diamond ameandika:

#Hallelujah ft @morganheritage LINK IN MY BIO! (Nyimbo hii ya #Hallelujah imenifunza kuwa uwoga wetu na kuto kujiamini ndio unatucheleweshea Mziki wetu Kuwa mkubwa Duniani… pia Umenifunza Ukithubutu kila kitu kinawezekana….Lakini pia Imenifunza kuwa wana Afrika Mashariki tuna nafasi nzuri ya kuweza kuvuma Duniani…. Imenifunza pia kuwa Hata Ukiimba Kingereza ila Nyimbo Ikiwa Nzuri Itapendwa na kuvuma kote Hadi Uswahilini……imenifunza pia kuwa Mwenyez Mungu hana Upendeleo ukijituma, Ukawa na nia nzuri na ukimuomba atakupa…. je wewe imekufunza nini?)