WEMA SEPETU AFUNGUKA ASEMA SIONI WIVU DIAMOND KUMKUMBATIA HAMISA MOBETO


Wakati habari zilizopo mjini kwa sasa ni tukio la mwanamitindo Hamisa Mobetto na msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ’Diamond’ kuteka tukio la utoaji tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF), kwa mrembo Wema Sepetu yeye kaichukulia kawaida.
Diamond na Mobeto katika tuzo hizo zilizofanyika jana ukumbi wa Mlimani City , walikwenda kama wageni waalikwa, walichaguliwa kukabidhi tuzo kwa mshindi wa kipengele cha ‘Best Original Music’ ambayo ilikwenda kwa filamu ya Safari ya Gwalu.
Katika kipengele hicho watu walikuwa wanasubiri kwa hamu kuona namna gani Wema ataweza kukabidhiwa tuzo na wawili hao, kwa kuwa filamu yake ya ‘Heaven Sent’ ilikuwa ni mojawapo iliyokuwa ikishindanishwa lakini bahati ndiyo hivyo haikuwa yake.

Akizungumzia namna alivyochukulia kitendo cha Mobetto na Diamond kufika eneo hilo na kuweza kukabidhi tuzo, Wema ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond miaka kadhaa iliyopita na hivi karibuni kuelezwa kwamba wamerudiana, amesema kitendo hicho kwake amekichukulia kawaida kwa kuwa Mobetto na Diamond ni mtu na mzazi mwenzake.
“Wee ulitaka nichukuliaje labda, Mobetto na Diamond hawa ni wazazi jamani , ulitaka nikasirike au,halafu isitoshe mimi sina uhusiano wa kimapenzi na Diamond bali ni washkaji tu na siyo kama watu wanavyosema,”amesema Wema.

Kuhusu hatua yake ya kupata tuzo mbili ya msanii bora wa kike na chaguo la watu (People’s Choice Award) kupitia filamu yake ya ‘Heaven Sent’, Wema amesema amefurahi kuona majaji wameweza kuona kipaji alichonacho.
Pia, aliahidi kuendelea kuwapa mashabiki wake kazi nzuri na kuwaondoa hofu wadau wa filamu waliokuwa wanasema kuwa bongo movie imekufa kuwa siyo kweli bali ilikuwa imelala tu.

Hata hivyo, hakusita kutoa shukurani kwa mashabiki zake ambao amesema ni kati ya watu ambao waliweza kushiriki kumpigia picha hadi kuhakikisha anapata ushindi huo.