Jina lake halisi ni Tatu Daniel , ila anafahamika zaidi kwa jina la Tantine- au jabuka jina alilolipata kutokana na filamu yake ya kwanza kabisa kuigiza iliyoitwa Jabuka . Ni mmoja wa warembo waigizaji wakubwa na wakongwe sana hapa barani ulaya na ameweza kujipatia heshima na umaarufu kutokana na filamu nyingi alizocheza .
AnaitwaClaurice Safi . Ni mmoja kati ya warembo wenye wa aina yake nchini na kwenye “industry” ya swahili movies. safi ni mwanadada mwenye mvuto unaokubalika na wengi na ameweza kujipatia kufanya vizuri kwenye filamu ya MY WIFE . Licha ya kuwa mwigizaji mwenye uwezo wa kipekee, Safi pia ni mwandikaji “script” mwenye viwango vya kimataifa.
Jina lake halisi anaitwa Ashey Toto na kisanii anajulikana kwa jina hilo hilo la Ashley. ni mmoja wa waigizaji wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya
swahili european movies
Ashley Toto
Jina lake halisi ni Abou Hemis Twaleb kwa mashabiki wake anafahamika kama “Abou”. Ni mmoja wa waigizaji na mmiliki wa kampuni ya filamu hapa Barani Ulaya. Alianza kama muigizaji na sasa anatengeneza, anaongoza Filamu na pia ni mwandishi wa “script” kwa ajili yake na watu wengine. Pia ni mshereheshaji (MC) kwenye shughuli mbalimbali za sherehe. Ni mchezaji mzuri wa mziki au dancehall.
Abou Hermis Twaleb
Devotha Alfred Anafahamika zaidi kama Rose ni mmoja warembo wenye mvuto wa pekee ndani ya tasnia ya europe movies kwa vipaji vyake vingi sana. Licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuigiza pia rose ni mwandishi na mwongozaji wa Filamu. Akiwa ameshaigiza kwenye zaidi ya Filamu nne) Pia Rose amesomea sanaa katika Chuo kikuu cha Mlimani Tanzania [fpa] Rose Pia ni mwanafunzi . Rose Hupenda kusikiliza muziki, kuogelea, na kusoma na kusafiri
Anajulikana zaidi kama “Mmewangu ” kama mwenyewe alivyopenda kujiita. Jina lake halisi ni Rizos Babingwa. Ni mmoja wa muigizaji na meneja mkubwa wa kundi la VAD . Na mmoja wa waanzilishi wa Swahili movies barani Ulaya , ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza ulaya kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza nchini Denmark, hasa Watanzania kama vile Lucy Komba , Mr nice , na wengine wengi. Rizos pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa wa Kigeni nchini. Moja ya filamu zilizompa umaarufu sana kama Nimwamini NANI , tanzania to Denmark
Rizo Babingwa
Akiwa mmoja wa waigizaji wa kike ndani ya Swahili european movies na mwenye umbo lenye mvuto. Blandine Wakengo ama blandine kama anavyofahamika na mashabiki wake ni mwigizaji aliyekuja kwenye tasnia ya filamu miaka ya karibuni na kuweza kujipatia umaarufu kupitia filamu mbalimabli alizoigiza.
Frank Salum
Big jj Olenga
sallai Majasiri
Jina halisi ni Sanura jafari sio jina geni kwa wapenzi wa vichekesho nchini kwani ni mmoja wa waigizaji wanaofanya vizuri sana kwenye tasnia hiyo .Pia ni mchekeshaji mkubwa sana.sanura anayekuja kwa kasi kwenye upande wa filamu na vichekesho
Anafahamika kama Mage seluwa ni mwanadada mwenye vipaji vingi ndani ya tasnia ya movies. Pamoja na kuwa mwigizaji aliyekuja kwa kasi sana pia mage ni mwanamuziki wa gospel fleva anayefanya vizuri sana sokoni kwa nyimbo zake mbalimbali zenye mahadhi mbalimbali. Pamoja na kuwa na umbo na sura nzuri ya kuvutia mage pia amekuwa akitawala sana vichwa vingi vya habari,magazeti na redio kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuimba nyimbo za injiri.
Mage Seluwa
Akiwa mmoja wa wasanii wanaofanya vizuri sana kwenye soko La Scandinavia movies nchini, Jina lake ni Papi Bin Gibril wake na kwa waigizaji wenzako anafahamika zaidi kwa jina la papi . Ameshaigiza kwenye filamu zaidi ya Tatu na kwa sasa ni Muheka hadhina wa kundi lake la VAD . Kwa upande mwingine ni Mwandishi wa stori .
Papi Bin Gibril
Jina lake halisi anaitwa Vumi Vane na kisanii anajulikana kwa jina hilo hilo la VUMI. ni mmoja wa waigizaji wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya SWAHILI movies
Gilbert Fatakid
Jina lake halisi ni Gilbert Fatakid ingawa wadau wengi wa movies wanamfahamu kama “ Gilbert ”, ni mmoja wa waigizaji chipukizi ndani ya tasnia ya filamu nchini. Pamoja na kuwa na mwili uliojengeka vizuri kimazoezi pia Gilbert Fatakid ni mwigizaji mwenye mvuto wa aina yake na ameweza kushiriki katika filamu chache hapa nchini. Anajulikana na mashabiki wake kama mwigizaji mstaarabu na mpole na mara nyingi kama mtu mwenye busara na maamuzi ya hekima.