Mwongozaji wa filamu maarufu nchini George Tyson Afariki dunia kwa ajali ya gari Morogoro

cvb1

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema mongozaji wa filamu maarufu nchini George Otieno Tyson (Pichani) amefariki dunia kwa ajali ya gari huko Morogoro.

 

Director mkubwa na aliye leta mapinduzi kwenye tasnia ya filamu Tanzania hatunaye tena..
Habari zilizo tufikia hivi punde ni kwamba GEORGE TYSON HATUNAYE TENA….amefariki kwenye ajari wakitokea Dodoma walipokuwa wamekwenda kufanya episode ya mboni show. Dereva alikuwa dj choka, abiria wengine ni mboni, zipompa, p funck, na dickson wa Eatv. Wengine majeruhi ila wengi wako safi tu taarifa zinaongezeka.

Taarifa hizi ambazo zimethibitishwa na watu wa karibu yake zinasema kuwa, mauti haya yamemfika baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali na kupinduka walipokuwa wameenda kwa ajili ya kipindi cha  The mboni show ambacho yeye alikuwa ndiye muongozaji mkuu.

Wasanii na mastaa mbalimbali nchini wameoneshwa masikitiko yako juu ya kifo hichi ikikumbukwa kuwa ni siku tano tu zimepita tangu mwigizaji Rachel Haule alipotutoka.

Batuli: – Niongee nini, niseme nini Mwenyezi Mungu tusamehe sie waja wako, Yarabbi eeeeeh Mola wng, R.I.P My brother, My shemeji, My director……Eeeeeh Mola mpokee George Tyson wetu, Poleni wasanii wenzangu, Poleni team nzima ya the mboni show thembonishow Pole Monalisa wangu

Rose Ndauka: Ki ukweli sina LA kusema ila asante baba wa mbinguni kwa kila jambo. …mola mpokee ndugu yetu, kwa mikono salama na umlaze pema peponi ameen…..R.I.P George Tyson.

Agness Masogange: R.I.P  George tyson mm siamin bado jmn E Mungu tuhurumie waja wako!

Flaviana Matata : This is very sad aisee,Rest In Peace Tyson.Mungu kakupenda zaidi, – monalisa pole sana dadangu,Mwenyezi Mungu awatie nguvu

Wema Sepetu – Kwa mara ya tatu bila hata kupumzika week… tunamzika mwenzetu mwingine… George Tyson…. Dah… Im just speechless.. RIP brother… Dah sijui Da Mboni wangu ana hali gani aisee…. Pole dada akee … Mungu akupe nguvu wewe pamoja na team yote ya @thembonishow …. Pigo kubwa tena kwa wasanii…. Tunaisha tu jamani.

Aunty Ezekiel – Mungu wang Naomba useme na sisi jaman Mungu baba tuone sisi jaman Naumia siwezi elezea jaman RIP Tyson wang jaman Rip director …..Nakosa lakusema

Mohamed Mwikongi : Hakika yametufika, A film director George Otieno Tyson naye hatunae tena duniani.

 

George Tyson aliwahi kuwa mume wa mwigizaji Monalisa na kuweza kuzaa naye mtoto mmoja. Mung ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :Bongo movie

Tupe maoni yako hapo Chini..!!

Hakuna Rap bila Fanatic sikia mashairi makali kutoka kwa aking Fanatic

Hakuna  Usafi bila maji , RAP bila fanatic hiyo ni mistali michache kutoka kwa King Fanatic bonyeza chini kusikiliza Ngoma yake kamili

10334247_510312839094283_3036561592813913663_n 10249708_493005194158381_2205424607189612266_n

https://www.youtube.com/watch?v=j1j75pQtB1s&feature=youtu.be

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :here

Tupe maoni yako hapo Chini..!!