MCHUMBA WA KUAMBIANA AJITOKEZA

Thursday, 23 May 2014

Na Vaida Duku

Siku mbili tu baada ya mazishi ya mwigizaji na mwongoza filamu mahiri Bongo, marehemu Adam Kuambiana, mrembo mmoja ameibuka na kusema alikuwa mchumba wa marehemu, Ijumaa linakujuza.Kwa mujibu wa Lulu Jumanne ‘Selina’, alifahamiana na marehemu Kuambiana mwaka 2006 akamwambia ndoa yake haipo sawasawa.
Alisema walianzisha uhusiano lakini haukuwa wazi katika jamii. Alisema siku moja akiwa anaishi Mwananyamala, wazazi wake walimtembelea.
“Nikiwa na wazazi nilimwona Kuambiana anapiga hodi, akaingia akiwa na  begi la nguo. Niliogopa kwani wazazi walikuwepo na walikuwa hawamtambui.k

“Hata hivyo, walielewa yakapita, tukawa tunaishi wote nyumbani kwa kupika na kupakua,” alisema Selina ambaye naye ni mwigizaji.
Aliendelea kuweka wazi kwamba, baada ya hapo maisha yaliendelea lakini ikafika mahali marehemu akahamishia mapenzi kwa Mbongo Fleva, Stara Thomas yeye akawa ‘zilipendwa’.

Akizidi kuanika mambo kuwa mwaka jana Kuambiana alirudi kwake baada ya kutofautiana na Stara, akataka waendelee na mapenzi yao na kumtambulisha kwa baadhi ya ndugu na marafiki

k2
 

Selina anasema alikuwa anafahamu kuwa Kuambiana alikuwa anaumwa tumbo kwa muda mrefu. Alikuwa akila chakula cha maelekezo ya daktari.
Hata hivyo, Selina alisema hapendi kueleza mengi lakini anaamini yeye ndiye mwanamke wa mwisho katika mapenzi na marehemu.

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :Dar kijiji

Tupe maoni yako hapo Chini..!!

 

Dr. Cheni amleta Mchina Bongo Movies. Mwenyewe adai biashara ngumu acha ajaribu fani

 

1425781_752263054788189_734834755_nBaada ya kumuingiza shabiki maarufu wa yanga football club “Steven” sasa Dr Cheni afanya mabadiliko makubwa ya bongo movie baada ya kumuweka mchina kwenye movie yake mpya.
Moja ya scenes ambazo mchina huyo amecheza ni sehemu ambayo amefumaniwa akiwa Guest. 
Tuliamua kumtafuta Mchina huyo Mr. Chaoxiang Deming ( 朝翔 德明  ) kujua kwanini kwanini amemua kujiingiza kwenye tasnia ya filamu nchini na alidai kuwa kwa sasa biashara imekuwa ngumu kidogo hivyo sio mbaya akajaribu kufanya mambo mawili matatu kuongeza kipato

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :bongo movies

Tupe maoni yako hapo Chini..!!