Actor Bigg jj Olenga Fighting against Ebola full video

Muigizaji na  Mkurugenzi wa kampuni ya filamu ya  Big jj  ,kutoka Denmark  Big JJ Olenga atoa wosia mkubwa juu ya ugonjwa wa Ebola, na kuwataka watu wafate maelekezo ya madaktari endapo watataka kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine , na kumalizia kuwa Mungu hatoangamiza binadamu kwa Maji wala kwa moto bali inawezekana kwa magonjwa kama haya yasiojulikana yametokea wapi.

665619_3756029665669_41386201_o
Bigg jj kwenye pozi

 

Swahili movies inampa hongera kwa kitendo chake hicho cha kutoa hiyo speech inaonyesha kiasi gani anavyojali binadamu au humanity na kuwataka sio tu waigizaji bali watu wote wenye uelewa wa  ugonjwa wa Ebola basi wawa elimishe wengine ambao hawajui lolote .

Big JJ akiwa kwenye Behind the scene ya badhi ya Filamu yake ghana

10626488_1450576698565426_8012747930440495668_n

Big jj akiwa kwenye Moja ya Filamu zake Denamark filamu ambayo very soon itaonyeshwa kwenye televison za Europe

 

10481933_719745231407712_9158947491068317358_o

on set

1614556_718057018243200_7583508649381484092_o

Bonyeza hapa kuangalia Video ambayo Big jj akiongelea Kuhusu Ebola

 

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :Here

Tupe maoni yako hapo Chini..!!

 

 

Siti Mtemvu ataka kujivua Taji la MISS TANZANIA Mwenyewe somahapa alichokiandika

1607042_692956617449081_2817346905523672701_n
MISS Tanzania 2014, Sitti Mtemvu juzi alilipua bobu la 2, baada ya kulazimisha safari ya kwenda kushiriki Miss World 2014 huku vigezo na masharti hasa yanayohusiana na cheti chake cha kuzaliwa yakipingana naye.

10387224_694715357273207_7158778018114358247_n

 

Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya Ukumbi wa Ngorongoro katika Hoteli ya JB Belmont, Posta Mpya jijini Dar es Salaam, Sitti alisema ana miaka 23 kwa kuwa alizaliwa mwaka 1991.
Pamoja na Lundenga kuweka wazi mchakato waliyotumia hadi kumfanya Sitti kuibuka na taji la Miss Tanzania 2014, bado kuna dosari za wazi ambazo zilijionesha kuwa mrembo huyo analazimisha safari hiyo kwani cheti chake cha kuzaliwa kinaonesha ana miaka 23 lakini namna cheti hicho kilivyotolewa ndiyo utata na ulazima ulipotokea.
Cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu.
Baadhi ya waandishi walimuhoji Sitti juu ya cheti hicho ambacho kinaonesha kimetolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Uzamini (RITA), Septemba  9, mwaka huu, siku 32 tu kabla ya kutwaa taji hilo.
Swali ambalo lilitawala kwenye kikao hicho lilikuwa ni kwa nini cheti hicho kitoke ndani ya muda mfupi wakati anaonekana alikuwa akiishi nje ya nchi kwa muda mrefu, na kwamba huwezi kuishi nje ya nchi bila paspoti ambayo pia upatikanaji wake unatakiwa kuwa na cheti cha kuzaliwa alisema kilipotea!
Akaulizwa alitoa ripoti kituo gani cha polisi ili waandishi waende kuulizia, akagoma!

 

BACKAMANI

“Mimi nadhani alichoongea Hashim Lundenga kinajitosheleza na zaidi naona mnanisakamasakama bila sababu ya msingi, nimechoka kuandamwa na vyombo vya habari pamoja na mitandao.
“Kama kuna mtu anaona cheti hakiko sahihi basi aende ofisi husika ili ajiridhishe juu ya hilo hata suala la kuniambia nina mtoto nafikiri mnaweza kwenda hospitali yoyote kuulizia hilo,” alisema Sitti.
..amekaa pembeni ili aweze kumfafanulia japo kwa ufupi juu ya mkanganyiko huo kama tangu alipomzaa Sitti hakuwahi kumchukulia cheti cha kuzaliwa hadi alipoamua kushiriki mashindano hayo.
“Mambo ya Sitti naomba muulize yeye maana ndiye mshiriki wa Miss Tanzania, mimi sijawahi kushiriki hata siku moja na hapa nimekuja kumleta yeye tu, hivyo siwezi kuzungumza lolote juu ya hilo, kikao hiki kimeandaliwa na Miss Tanzania na si ukoo wa Mtemvu,” alisema mama huyo.
Hili ni bomu la pili, la kwanza ni lile lwa kudai ana miaka 18 siku alipojitambulisha kwenye shindano hilo, Mlimani City, Dar na kuzua utata mkubwa kwenye jamii.
Baada ya kuaona kuwa anaandamwa hiki ndio alichokisema mrembo huyo
10363809_305092086341540_3363722063330340080_n
Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT : GPL

Tupe maoni yako hapo Chini..!!