Category Archives: Swahili

kumekucha V.A.D Waja na sehemu ya nne Episode ya nne ya Tamthilia ya MAWENGE ; WASANII WAPYA NDANI

Wale wakali wa filamu na Tamthilia za kiswahili kutoka nchini Denmark waja sasa na sehemu ya nne ya tamthilia yao inayoendelea youtube ya MAWENGE tarehe 06.04.2019 kama kawaida imejaa wasanii maarufu löakini pia sura mpya yaani waSANII WAPYA kabisa tegemea kuwaona toka tamthilia ya mawenge.
Swali tunayo kwa nini roho za YUDA na KAINI uendelea ku tawala na kuongezeka jamani? watu tujifunze kuwa na roho za uruma na tusijipende wenyewe bonyeza link chini kucheki tamthilia hio ya mawenge au waeza watafuta youtube kwa jina la kampuni yao VAD FILM PRODUCTION

walie cheza ni wasani kutoka inchini Danmark kundi la V.A.D the voice of africa in Denmark
Ndani ya EPISOD iyo utakutana naye Lucy Komba, Selembe Toko, Safi Happy, Kay Msabaha, Safari Lukeka, Tatu Musa, Agnes Sakina na wengine wengi/54279298_435392997202701_9145456304993599488_n.png” alt=”” width=”960″ height=”540″ class=”alignnone size-full wp-image-4779″ />

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXHURUMA :Baba OMMY DIMPOZI ADAI KATELEKEZWA NA MWANAE

Pichani mwenye tshet nyekundu ni baba yake mzazi Ommy Dimpoz ambapo Amesema mwanae huyo amemtelekeza miaka Mingi licha ya Dimpoz kusifika kwa kula bata nchi mbalimbali duniani. Baba Dimpoz Ana miaka 64 na ni dereva wa bajaji huko Tabora. Babaji amenunua mwenyewe. Wanaomjua wamesema anashindia mihogo na kachumbari !!

Mzee Faraji Nyembo akizungumza na Globalpublishers anasema

“Ni kama Wema Sepetu anavyohangaika kutafuta mtoto, siku akimpata hata kama hamsaidii chochote atamshukuru tu Mungu hivyo na mimi huwa ninamshukuru Mungu maana nimeshamleta Omary duniani. Yeye kama mtoto, ndiye anayetakiwa kujua mzazi wake anahitaji nini, yaani ukimuuliza sasa hivi Dimpoz akupe namba yangu, utaona, atakujibu nini maana ninaamini hana. Nimekuwa nikimpigia, lakini simu yake unaambiwa inatumika, angekuwa anaona umuhimu si angekuwa na namba maalum kwa ajili ya kuwasiliana na mimi baba yake kama mastaa wengine wanavyofanya kuwa na namba kwa ajili ya mashabiki na nyingine ya watu muhimu,” alisema na kuongeza

“Mfano nikifa kama leo ni bora huyo Ommy asinizike au kuja Tabora maana watu watampiga na kwanza atasema ni nani wake amefariki dunia maana hivi niko hai hana ushikiano,” alisema baba huyo.

Ommy Dimpoz ambaye amelelewa upande wa mama yake alipotafutwa na GPL hakujibu kitu kuhusu madai ya Baba yake huyo

CREDIT :TRIM SALEEM ;GLOBALPUBLISHER

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX