PAUL MAKONDA ANASEMA HATAUSAHAU MWAKA 2017,MWAKA WA MISUKOSUKO KATIKA MAISHA YAKE


“Mwaka 2017 ni mwaka watofauti sana kwangu. Leo tunapojiandaa kupokea Mwaka 2018. Ni vyema nikayatazama maisha yangu ndani ya mwaka 2017 hakika huu ulikuwa mwaka wa aina yake. Ni mwaka ulionipa marafiki wa kweli, lakini kubwa kuliko ni Upendo na Maombi niliyoyapata kutoka Kwa Kipenzi changu Maria. Nikuambie kitu ndg msomaji…… haikuwa rahisi kama siyo Mungu kuwatumia wateule wake sijuwi leo nigekuwa wapi. Nimepewa kila jina baya, kila jambo baya nimefanya mimi ,matusi yote yalikuwa yangu na hata watu kutamani nisiwepo duniani. Lakini kwako Mpenzi ilikuwa tofauti, ulinitia moyo Kwa sauti ya upole,uliniombea na kunifuta machozi bila kuchoka. Tena Kwa kusema Nanukuu, Paul Mungu hajawahi kukuacha hata kama Dunia yote inakuona haufai nataka nikuambie Mungu amekupaka mafuta Kwa kazi hii simama na usonge mbele. Mwisho wa kunukuu”.Ndg zangu na wananchi wenzangu ni vyema mkajua kila mtu anayo hadithi ya kumweleza mwenzake ila kwangu inahitaji kitabu kuyaeleza mapito na njia nyembamba niliyoipita mwaka 2017. Itoshe kusema Mungu wa haki iko siku atasimama na kutoa hukumu ya kweli Kwa watu wote. Kwani yeye anatujua kila Mtu na matendo yetu tena kwake hakuna Siri ya maisha yetu.Nakupenda sana Maria wangu na ninathamini sana Mchango wako ktk utumishi wangu hapa Duniani. Uzidi kuwa Imara simba wangu ili niyafanye yote mema ambayo Mungu amepanga Kwa watu wake. Asante sana Mungu Kwa kunivusha mwaka 2017.”

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxhttps://www.youtube.com/watch?v=vaDxb11G_lo&t=543shttps

Huu ndio Ujumbe wa zari the bossylady wa mwaka mpya kwa wote wanaomchuki utacheka!

Licha ya kuandika jumbe mbalimbali za kuiuaga mwaka mpya zari amemaliza kwa kuandika ujumbe huu kwa watu wote wanaomchukia lakini bado kila kukicha wamekuwa wakimuandika kwenye instagram page zao

swahili news inawatakia heri ya mwaka mpya wote .

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx