Niliokoka baada ya kuigiza kama yesu kwenye filamu ya YESU :Actor Brian Deacon

 

jfp15a_jesusfilmproject_web

Katika kipindi cha  kuelekea siku kuu ya Pasaka au christmass, ni jambo la kawaida kukuta nyumba za waumini wa dini ya Kikristo zikiwa zimepambwa na picha mbalimbali za Yesu, lakini pia kama wewe ni muumini wa dini hiyo, unapotajiwa au kulisikia jina la Yesu, kuna picha fulani inakujia mawazoni, kuna sura fulani inakujia mawazoni, si picha au sura nyingine, bali ni sura ya Yesu.

Brian_Deacon-3
Brian Deacon katika filamu ya Yesu

 

Wapo wanaodhani kuwa picha hiyo au sura hiyo ndiyo Yesu mwenyewe aliyezaliwa yapata miaka 2000 iliyopita, hapana, hakuna anayejua sura ya Yesu ikoje, anaonekana vipi, bali mtu huyo ambaye ulimwengu umezoea kumwona kama ndiyo Yesu wa Nazareti, huyu ni jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Brian Deacon, huyu ndiyo jamaa aliyeigiza ile filamu maarufu ya Yesu, inayojulikana kwa jina la ‘Jesus Film’ mwaka 1979. filamu hiyo iliigizwa na watu mbalimbali ambao wengine wapo hai mpaka leo, picha za filamu hiyo zilipigwa nchini Israeli.

3872875
Kutoka kushoto ni Dalia Shapira aliyeigiza kama Mary Magdalene, Babi Neeman aliyeigiza kama Yakobo, Niki Mitai aliyeigiza kama Petro na Brian Deacon aliyeigiza kama Yesu katika filamu hiyo
4994605
Katikati ndiyo Brian Deacon aliyeagiza kama Yesu, Kushoto ni mmoja wa watoto wa waigizaji katika filamu hiyo aliyeigiza kama Yesu mtoto na kulia alieyeigiza kama Yesu mwenye umri wa miaka 12

Je Brian Deacon ni nani?

Brian Deacon ndio jina halisi la mwigizaji huyo ambaye ni raia wa Uingereza alizaliwa tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza ni mtoto wa pili katika familia yao, baba yake alikuwa ni fundi makenika huku mama yake akiwa akiwa ni Muuguzi.

untitledimages

   Brian Deacon aliyegiza kama yesu katika filamu ya Yesu
Maisha yake ya Ndoa
Brian alifunga ndoa yake ya kwanza na binti aliyejulikana kwa jina la Rula Lenska mwaka 1977 na kufikia mwaka 1987 ndoa hiyo ilivunjika, huku wakiwa wamefanikiwa kupata mtoto wa kike ajulikanaye kwa jina la Lara Deacon,
Mwaka 1998 alifunga ndoa nyingine baada ya kuachana na Rula, alimuoa Natalie Bloch ambaye yupo naye mpaka sasa.
Brian_Deacon

Jesus-Film-PR-3

Filamu

Alipata nafasi ya kuigiza filamu ya Yesu baada ya kupita mchujo, katika mchujo huo walijitokeza waigizaji zaidi ya 1000. Brian Deacon aliwahi kunukuliwa akisema kuwa, filamu hiyo ya Yesu ilimfanya yeye kuokoka baada ya kuitamaza kwani kabla ya kuigiza filamu hiyo hakuwa ameokoka. ilichukua miezi saba Mpaka filamu hiyo inakamilika

Filamu nyingine alizowai kucheza ni kama    A Zed & Two  ( 1985),       Vampyres   ( 1974 ),    The Triple Echo   ( 1972)  ,  Lillie (1978)

SOURCE  : venancefuraha.blogspot

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

 

Tupe maoni yako hapo Chini..!!

Imeandaliwa na Furaha Venance, Habari na picha kwa msaada wa Mtandao

 

UNATAKA WACHEZE FILAMU YAKO? ANDAA MKWANJA HUU

LUCY MGINA
KILA mwanamichezo au mwanamuziki hulipwa mshahara kulingana na kiwango chake, hali hii ipo hivyo pia kwa waigizaji na watu wengine wa kawaida.
Hali hii imekuwa ikiwapa morali zaidi wale wanaofanya kazi kujituma ili wapate mshahara mkubwa zaidi au kupewa kazi ya ziada tofauti na pale ulipozoea.

RAY

Hii pia imekuwa ikifanyika kwa wasanii wa filamu za Tanzania wenye umoja wao maarufu kama Bongo Movies. Hao wamekuwa wakilipwa madau kama wachezaji ili wafanye kazi za wenzao, hii imekuwa ikileta changamoto kubwa kwa wasanii kuhakikisha wanapanda dau kutokana na uwezo binafsi.

Asilimia kubwa ya mashabiki wa filamu za kibongo wamekuwa wakitoa fedha za kununua kazi zao bila kufahamu muhusika ‘anayemnunua’ amelipwa kiasi gani cha fedha kucheza ‘movie’ aliyoinunua. Tazama bei zao hapa chini:

Vincet Kigosi ‘Ray’
Inadaiwa kuwa huyu jamaa ni mgumu sana kukubali kucheza filamu za watu. Alishawahi kupewa Sh Milioni 10 ili cheze filamu moja (jina kapuni) lakini aligoma na amekuwa na msimamo mkubwa katika kazi zake lakini badala yake hizo fedha zikawalipa wasanii wengine watatu.
Inaaminika ndiye msanii mwenye gharama kubwa licha ya kuwa mpaka sasa bado amekuwa akigoma kucheza filamu za wenzake, ishu kubwa akidaiwa kujiona ni ‘staa’ zaidi ya wenzake.

10570231_500727066740183_808236221_n

Wema Sepetu
Kipaji chake kiliibuliwa na marehemu Steven Kanumba kupitia Filamu ya ‘A Point Of No Return’ baada ya hapo akapata mashavu kibao na hadi sasa amefanikiwa kucheza filamu na msanii mkubwa Van Vicker raia wa Ghana.
Za mjini zinasema kabla hajaachana na aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wake, Clement alikuwa akitoza kuanzia Sh Milioni Tano kwa filamu moja lakini sasa anapokea hata chini ya hapo kwa kuwa fedha zimeanza ‘kumkatikia’.
Wema ambaye pia ni Miss Tanzania mwaka 2006, alizaliwa mwaka 1988, Dar anamiliki kampuni yake inayofahamika kama Endless Fame Films na ndiye mkurugenzi mtendaji.

IMG_4198

Kajala Masanja
Ana kampuni yake ya uzalishaji wa filamu inayoitwa Kay Entertainment na tayari ameshafanya kazi zake zinayofahamika kwa majina ya Mbwa Mwitu pamoja na Pishu.
Lakini linapokuja suala la kufanya kazi za watu inakulazimu kuzama katika pochi au ‘waleti’ ukitoa mkono uwe na Sh Milioni Mbili lakini kwa kiasi hiki awe anakufahamu na kama ‘ndo’ mnaona kwa mara ya kwanza jiandae kuachia Sh Milioni Tatu hadi 2.5 zaidi ya hapo hakuna maneno maneno kazi inapigwa kwa kiwango kikubwa tu na binti huyu aliyezaliwa mwaka 1983.

JacklineWolper2

Jacqueline Walper ‘Wolper’
Ninja, dada mkubwa, anaweza kucheza ‘sini’ zote ziwe za kijambazi, mke mwema na hata changudoa, amekuwa na mashabiki wengi sana Bongo na hata nje ambao wamekuwa wakipenda kazi zake.
Mshkaji huyu ambaye alizaliwa mwaka 1987 huko Moshi, Kilimanjaro, yupo kishkaji tu kwani anakubali kupokea kuanzia Sh Milioni 2 hadi 2.5 hapo haipungui labda iongezeke ndipo atakufanyia kazi zako. Mpaka sasa amecheza filamu zaidi ya 20.

 

207746_194098800625533_1630776_n

 

Mzee Majuto
Licha ya kuzaliwa mwaka 1948 huko Tanga, Amri Athuman ‘King Majuto’ au Mzee Majuto bado inaaminika kuwa ndiye msanii mwenye mashabiki wengi zaidi Bongo kutokana na uimara wa kuigiza hususan kwenye filamu za kuchekesha.
Mzee wa watu hana makuu ukitaka achekeshe weee filamu nzima jiandae kumkatia Sh Milioni 1.5 hadi 2 tu, hicho ndicho kiwango chake na atakufanyia kazi kwa umakini mkubwa zaidi ya hapo hashuki. Nje ya fani anamiliki daladala mbalimbali huko kwao Tanga ambazo pia zinamuongezea kipato

riyama

Riyama Ally
Anaigiza kwa hisia kali sana katika kila filamu, ukitaka alie na machozi yatoke kwa wingi au acheze filamu za kimbea, majungu, vigodoro na nyinginezo wala hana makuu dada wa watu anapokea hata Sh Milioni 1.5.
Riyama ambaye alianza kujihusisha na maigizo mwaka 2000 akiwa na kundi la Taswira, mara nyingi katika filamu alizocheza anasifika kwa kuigiza kwa uhalisia mkubwa pengine ukimtoa Johari wa enzi za Tamthilia ya Johari basi huyu ni namba mbili kwa wepesi wa kutoa machozi. Mpaka sasa amecheza  filamu zaidi ya 40.

joha
Blandina Chagula ‘Johari’
Alipata jina kupitia Tamthilia ya Johari kabla ya kuhamia kwenye filamu. Ni Mkurugenzi wa Kampuni ya RJ akisaidiana na msanii mwenzake Ray, katika kuindesha. Diva huyu wa movie za Kibongo alizaliwa mwaka 1983 huko Shinyanga.
Hana makuu katika kusaidia wenzake na mara nyingi amekuwa akijitoa kwa moyo kucheza filamu yoyote. Dau lake ni la ki-upendo zaidi kwani anapokea hata Sh Milioni Moja, hii yote anafanya kwa lengo la kusaidia wenzake. Anasifika zaidi kwa kucheza filamu za kulialia kwani kwake kutoa machozi si lolote hata sekunde mbili hazipiti anakuwa kayatiririsha hatari.

SOURCE  :global publisher

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

 

Tupe maoni yako hapo Chini..!!