Mwanamziki Ma-jadee kushare stage na kanda king na kanda Junior Mwezi Ujao hakika si ya kukosa

10389234_10203116851657997_1674787157749117854_n

Mwanamziki Sexy lady  Ma-jadee mkenya mwenye makazi yake Germany amethibitisha kuwa ataperform pamoja na wanamuziki kutoka kenya ambao ni Kanda King na Kanda Junior huko Mjini Frankfurt Germany  mapema mwezi December ,

na kuwataka amshabiki wake wasikose katika kusherehekea   kenya Independency day , si tu wakenya pia amewakaribisha watu wote waweze kusherehekea kwa apaoja na kusema siku hiyo atapiga show ya kufa mtu ……Alimaliza mrembo huyo ambaye kwa sasa anatamba na ynimbo yake ya  NITASEMA ICHEKI HAPO CHINI.

 

 

10701992_1480141752270360_9165045157593731613_n

 

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :Here

POSTED BY : Hamm Chande

 

Bi harusi apewa talaka siku ya harusi

 

141118122527_saudia_512x288_bbc

 

Bwana harusi mmoja kutoka Saudi Arabia amempa talaka mkewe siku ya harusi baada ya kumuona uso wake kwa mara ya kwanza wakati mpiga picha alipotaka kuwapiga picha.

Maharusi hao kutoka mji wa magharibi wa Saudia,Medinah walikubaliana kuoana licha ya kutoonana uso kwa uso,swala ambalo ni utamaduni mkubwa wa mataifa ya mashariki ya kati.

lakini wakati mwanamke huyo alipofungua kitambara alichokuwa amejifunika uso na kutabasamu katika kamera,mumewe alishtuka na kuondoka wa ghafla.

Kulingana na gazeti moja katika eneo hilo kwa jina Okaz,mwanamume huyo alianguka na kuzirai huku wageni waalikwa wakijaribu kuingilia kati ili kutatua kilichokuwa kikiendelea.

Hatahivyo Bwana harusi alisema kuwa hakuweza kumwona bi harusi kabla ya harusi yao gazeti hilo la Okaz liliripoti.

” Si wewe msichana niliyetaka kuoa,si wewe kamwe niliyedhani ” kwa hivyo nakupa talaka”alisema bwana harusi.

Na alipompa talaka bi harusi naye alianguka na kuzirai na kuifanya harusi hiyo kuwa usiku wa majonzi.

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :http://www.bbc.co.uk/

POSTED BY : Hamm Chande

Tupe maoni yako hapo Chini..!!