Actress Marian Rivera Withdraw from her upcoming Drama because of the pregnancy

darna

Kama anavyojulikana na wengi  kAPUSO Queen Marian Rivera star wa filamu na Tamthilia mbalimbalia kama , DARNA , AMAYA, Djesebel  na nyingine nyingi ndoa yake aliyofunga na muigizaji mwenzake mkubwa wa ufilipino Dingdong Dantes mwezi wa kumi na mbili ndoa hiyo iliyokuwa na keki iliyovunja rekodi kwa ukubwa duniani, ameamua kukatisha mkataba wake wa tamthilia mpoya aliyokuwa ameanza kuicheza  ya RICHMANS DAUGHTER Baada ya kutangaza kugundua kuwa ni mjamzito mapema wiki  hii  na taarifa hizo kupokelewa kwa maskitito na mashabiki wake .

amaya_marian_rivera-copy

Marian Rivera has withdrawn from her upcoming GMA-7 primetime Drama “The Rich Man’s Daughter” after announcing her pregnancy earlier this week.

GMA Network confirmed the development in a statement on Friday, adding that the Kapuso Primetime Queen will also not be joining her scheduled GMA Pinoy TV guestings abroad “due to her delicate condition.”

amaya-twin-snake5-copy

“GMA Network fully supports Marian’s decision and strongly believes that Marian and her baby’s safety is first and foremost,” said the network.

Marian had previously expressed excitement over her new show because of it’s theme, which features her as a woman in love with another woman.

dyesebel

GMA-7, meanwhile, assured fans that Marian will continue to appear in various shows on the network.

“We pray for a healthy and happy pregnancy for our dear Marian,” it said. — JST, GMA News

media_httpandronicofi_shqhf

KUWEZA KUTAZAMA TAMTHILIA HIZI MATATA ZA KIFILIPINO NA NYINGI ZAIDI ONLINE TEMBELEA

Website: VIKI.COM

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :  http://www.marianriveradantes.com/

The Official Facebook Fan Page of Marian Rivera Gracia-Dantes.

Tupe maoni yako hapo Chini..!!

 

 

Mauaji ya wageni south Africa yapamba Moto Boko Haram yaipa masaa 24 south Africa kumaliza Xenophobic

Chama tawala nchini Afrika Kusini African National Congress ANC kimelaani wimbi la mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni ambayo yamesababisha vifo vya watu sita na kusababisha hali ya wasiwasi nchini humo

0,,18383941_403,00

Taarifa kutoka kwa chama cha ANC imesema katika kipindi cha majuma kadhaa sasa, taifa la Afrika Kusini limeghubikwa na wimbi la mashambulizi ya kufedhehesha yanayowalenga raia wa kigeni kutoka nchi nyingine za Afrika.

ANC imeyataja mashambulizi hayo vitendo vya kihalifu dhidi ya watu wanyonge ambao wanatafuta hifadhi, faraja na kujiendeleza kiuchumi na kuongeza raia wa kigeni hapaswi kulaumiwa kwa changamoto zinazowakumba raia wa Afrika Kusini.

Katika mji wa kusini mwa nchi hiyo wa Durban mashambulizi yaliyochochewa na chuki dhidi ya wageni yamezilenga biashara na makaazi ya raia wa kigeni wakiwemo kutoka Somalia, Ethiopia na Malawi licha ya polisi kuimarisha doria katika mji huo kuzuia mashambulizi hayo.

Rais yuko kimya

Taarifa hiyo kutoka kwa ANC inakuja baada ya shutuma kuwa Rais Jacob Zuma ameshindwa kutoa tamko hadharani kuyalaani mashambulizi hayo. Mapema mwaka huu, raia wa kigeni pia walishambuliwa na maduka yao kuporwa katika kitongoji cha Soweto kilichoko karibu na mji wa Johannesburg

0,,18257691_403,00

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Mashirika ya kutoa misaada yamesema zaidi ya raia 2,000 wa kigeni wameutoroka mji wa Durban wakihofia maisha yao na sasa wanaishi katika kambi za muda chini ya ulinzi wa polisi na iwapo mashambulizi hayo hayatasitishwa,idadi ya waathiriwa inatarajiwa kuongezeka.

Mhamiaji mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Johnny ambaye ni raia wa Zimbabwe anasema anatafakari kurejea nyumbani

Jana maduka mengi yalifungwa katikati mwa mji wa Johannesburg baada ya wafanyaibishara kuhofia ghasia zitazuka baada ya vitisho kusambazwa katika mitandao ya kijamii.

Msumbiji imetangaza inapanga kuwasaidia raia wake walioko Afrika Kusini kurejea nyumbani baada ya waziri wa habari wa Malawi Kondwani Nankhumwa kusema wanawarejsha nyumbani raia wao 400 waliochomewa nyumba na mali zao. Malawi ndiyo nchi ya kwanza ya Afrika kuwaondoa raia wake kutoka Afrika Kusini.

safrica6-e1422251799388

Mfalme anashutumiwa kuchochea chuki

Mfalme Goodwill Zwelithini kiongozi wa kabila kubwa zaidi nchini Afrika Kusini la kwa Zulu Natal anashutumiwa kwa kuchochea mashambulizi hayo baada ya kutoa hotuba wiki mbili zilizopita akiwataka raia wa kigeni kufunga virago na kurejea makwao

Mwakilishi wa mfalme huyo Thulani Zulu amekanusha kuwa mfalme huyo ndiye aliyechochea mashambulizi hayo na kuongeza kuwa amesikitishwa na yanayojiri na anayalaani .

Wanaharakati wanaopinga chuki dhidi ya raia wa kigeni wanapanga maandamano makubwa mjini Durban hii leo kuishinikiza serikali kuchukua hatua zaidi kuwalinda wahamiaji. Polisi Afrika Kusini imesema imewakamata watu74 kuhusiana na mashambulizi hayo.

0,,18383939_403,00

Raia wa Afrika Kusini ambao hawana ajira wanawashutumu wageni kuwa wanachukua nafasi zao za kazi. Mwaka 2008, watu 62 waliuawa katika mitaa ya Johannesburg kutokana na chuki hizo dhidi ya wageni.

WAKATI HUO HUO BOKO HARAM

Boko haram wameachia video ikiwataka wasouth Africa wastopishe mauaji hayo ya wageni haraka iwezekanavyo ndani ya masaa 24 vinginevyo watashughulika na raia wa kisouth africa wanaoishi nchi nyingine za Africa kama CHAD , Nigeria na nyinginezo ikiwemo balozi za south Africa.

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT : BBC

Tupe maoni yako hapo Chini..!!