Monalisa :Wasanii Wanajiachia Sana

 

MONALISA45

YVONNE Cherryl ‘Monalisa’ mwigizaji wa kike katika tasnia ya filamu Swahilihood amefunguka kwa kuwaambia baadhi ya wasanii katika fani ya uigizaji kushindwa kulinda miili yao na kujiachia kwa kunenepa na kupoteza muonekano wao jambo ambalo linapoteza nafasi zao katika sinema.

“Sisi wasanii wa filamu kwa Bongo hatuwezi kabisa kulinda muonekano wetu kimaumbo msanii akikubalika tu anajiachia mwili huo, vijana wadogo tu kuna wakati unashindwa umchezeshe kama binti au mama mtu mzima, lakini ukimuona msanii kama Sarafina yupo vile vile,” anasema Monalisa.

Monalisa anasema kuwa moja kati ya vitu muhimu katika tasnia ya filamu ni kuwa na mpangilio wa vyakula kufanya mazoezi ili kuendelea kuwa katika muonekano mzuri kama vile akina Angelina Jolie walivyodumu na hata badhi ya wasanii wengine Afrika ambao hawajapoteza mvuto kwa kujiachia kunenepa bila mpangilio.

 

SOURCE  : bongo movies.com

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

 

Tupe maoni yako hapo Chini..!!

 

Shamsa Ford: Mchawi wa Maisha Yako ni Wewe Mwenyewe

SHAMSA_87

 

NIDHAMU ni silaha kubwa katika maisha.kuna ambao Mungu aliwabariki kwa nafasi zao lakini hawakuweza kutumia nafasi zao vizuri kwasababu ya kukosa nidhamu.walihisi wao ni bora kuliko wengine ndo maana walibarikiwa.

Mwisho wa siku wakishapotea au mambo kwenda tofauti na walivyokuwa wanadhania wanaanza kulaumu watu.Wengine wataingia hadi kwenye ushirikina kwa kusemwa wamerogwa..Mchawi wa maisha yako ni wewe mwenyewe…MUWEKE MUNGU MBELE,KUWA MVUMILIVU,ACHA TAMAA,FANYA KAZI KWA BIDII, PENDA KUJIFUNZA NA KUBALI USHAURI

Shamsa Ford “@shamsaford” on instagram

SOURCE  :Bongo movies.com

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

 

Tupe maoni yako hapo Chini..!!