Mastaa wa filamu nchini King Majuto, Irene Uwoya, Vicent Kigosi “Ray”na Jacob Stephen(JB)
Wanatarajia kuondoka Tanzania usiku huu kwenda nchini Uturuki kwa ziara maalum ya kikazi ambayo imedhaminiwa na Princess Casino iliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es salaam Tanzania na wamiliki wenye asili ya Uturuki. Wasanii hao wakizungumza na media leo walisema kuwa kwa mujibu wa wenyeji wao watakutana na mastaa wa filamu na watu muhimu nchini humo na kujifunza tamaduni zao na pia kukuza wigo zaidi wa kazi za filamu za Tanzania. Ziara hiyo ni ya wiki moja.
Hili ni jambo jema kwa wasanii wetu kuonyesha kuwa tasnia na wasanii wetu wanatambulika. Pia ni matumaini yetu kuwa wasanii hawa wataenda kuutangaza utamaduni wa Tanzania nchini humo na sio wao kujifunza utamdun i wa nchi hiyo pekee.
Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more
CREDIT : Bongo5