Chidi Benz akamatwa na dawa za kulevya airport.

Chidi Benz amekamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa anaelekea jijini Mbeya kwenye show ya Instagram Party inayotarajiwa kufanyika kesho.

Chidi-Benz-12
Chizi Benz

Chid-Beenz_full

Akizungumza na tovuti ya Bongo5 leo msanii Shetta ambaye alikuwa naye pamoja katika safari hiyo ya kuelekea Mbaya, amethibitisha kukamatwa na kwa Chidi akiwa na vitu vinavyohisiwa ni madawa ya kulevya.

“Kweli tulipata matatizo na Chidi pale airport ila mimi nikaruhusiwa yeye nikamuacha, amekamatwa na mambo mambo fulani sema ongea na wahusika watakwambia zaidi,” alisema Shetta.

Akizungumza na Millard Ayo, kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi Selemani kamanda wa polisi katika uwanja wa ndege Dar es Salaam amesema Chidi Benz amekiri kuwa dawa hizo ni zake.

Amedai kuwa Chidi alikutwa na kete 14 za dawa za kulevya pamoja na misokoto miwili ya bangi iliyokuwa mifukoni mwake.

Chidi atapandishwa mahakamani hivi karibuni kwa kosa la kukutwa na dawa hizo.

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT : Bongo movies

Tupe maoni yako hapo Chini..!!