Hamisa Mobeto aumbuka APEWA ONYO KALI NA DANUBE

Hamisa Mobeto aumbuka !! Wanasheria wa kampuni ya Danube wadaiwa kumtumia Hamisa barua ya kumtaka afute video ya Zari na Diamond aliyopost wiki chache zilizopita katika akaunt yake. Kwa mujibu wa barua hiyo ambayo imeanza kusambaa Danube wamesema Hamisa sio balozi wa kampuni Yao na wala hawafanyi nae kazi kwahiyo alipost official video ya tangazo la kampuni hiyo kwa manufaa yake binafsi na sio kampuni ambapo katika video hiyo Diamond na Zari wanatangaza bidhaa za kampuni hiyo huku Zari akizungumzia mambo ya hereni. Barua hiyo inaonekana ni ya tarehe 9 October 2017.

Hata hivyo Hamisa tayari amefuta video hiyo ambayo aliipost huku kukiwa na mkorogano mkubwa baada ya habari za kuzaa and Diamond. Haijaeleweka nani amevujisha mitandaoni barua hiyo ambayo mlengwa ni Hamisa kwani wengi walidhani Mobeto alilipwa na kampuni hiyo kupost tangazo hilo

Nini maoni yako ?