Baba Diamond Afunguka mkewe bi sandra kuolewa na kibet ten

Mzee Abdul baba mzazi wa Diamond amesema hata yeye kwasasa ana mtu wake mpya, awaka na kuja juu baada ya kuulizwa kuhusu Dr.Sandrah kuolewa na kibenten
.
Baada ya baadhi ya wapenda ubuyu wa mastaa kutaka kusikia kauli yake baada ya mzazi mwenzie kuolewa, mapaparazi wa GPL walipomfuata ndipo akawacharukia mapaparazi kwa kusema

.
“Sitaki hata kuwasikia. Naomba tuheshimiane, nimesema sitaki… sitaki…sitaki kuwaona hapa nyumbani kwangu, ondokeni. Tusitake kuharibiana siku hapa,”
.
Baada ya kuambulia patupu, mapaparazi hao walienda kujipanga upya kuongeza nguvu na mbinu za kumshawishi baba Diamond na Safari hii akatulia na kugunguka haya
.
“Jamani sililizeni kwani mnanitafutia nini? Tatizo ni nini kwani Bi Sandra akiolewa? Hivi mlitegemea atakaa vilevile hadi lini?, Mimi huku nina mtu wangu, tuna maisha yetu, sasa mlitegemea yeye akae mpweke hadi lini? Haya ni maisha na kila mtu anaamua kuishi anavyotaka kwa hiyo mimi sioni tatizo hata kidogo,” alisema Mzee Abdul.
.
Alipoulizwa kuhusu kumuonea wivu Shamte ambaye ndie mume wa sasa wa Bi.Sandrah kwa raha anazoponda amejibu
.
“Hiyo ni riziki yake. Kama yeye anakula raha, sawa, ndiyo riziki yake Mungu amemuandikia. Mimi nimeridhika na maisha yangu hayahaya ya kawaida,” alisema Mzee Abdul akimtakia Bi Sandra kila la heri kwenye maisha yake mapya ya uhusiano na Shamte akimalizia kuchonga na GPL
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
KUFATILIA MAISHA YA UGHAIBUNI SUBSCRIBE KWA VLOGERS HAPA CHJINI KUONA VIDEOZ ZAO ZOTEE: