BABA KANUMBA AIBUA MAPYA KWA waziri MWAKYEMBE


BABA wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba ameibua mapya kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe baada ya kumwangukia na kumuomba asimsahau katika mikataba aliyosaini mwanaye.

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa nyumbani kwake Shinyanga, baba Kanumba alisema anamuomba waziri huyo amsaidie ili aweze kupata haki yake kama mzazi endapo mikataba ya kazi aliyoingia mwanaye enzi za uhai wake itafanikiwa.

Aliendelea kusema kwamba anaiomba serikali iingilie kati suala hilo na endapo fedha hizo za mikataba ya Kanumba zitatoka basi wasaini wote yeye na mama Kanumba na siyo waangalie upande mmoja yaani mama tu.

Namuomba sana Mwakyembe anikumbuke na mimi kwenye kusaini fedha za mikataba ya mwanangu iwapo zitatoka kwani nami nina haki maana nilimlea sana akiwa mdogo mpaka akawa mkubwa nikamuuliza anachagua kukaa wapi ndipo akachagua kwenda kuishi kwa mjomba wake. “Kwa sasa mimi nimekuwa mlemavu wa miguu hivyo naomba na mimi nikumbukwe, na mimi nina haki msinisahau,” alisema baba Kanumba.

Baba Kanumba ameya-zungumza yote hayo ikiwa ni baada ya hivi karibuni Waziri Mwakyembe kuzungumza bungeni kwamba watashughulikia mikataba ya kazi waliyoingia wasanii kama Mzee Majuto na Kanumba ili waweze kupata haki zao

STORI: Gladness Mallya, Risasi Mchanganyiko

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx