Ndoa ya Ustazi Juma na Johari yanukia. Asema Johari atakuwa mke wake wa pili

bbbnJohari na Ostadh Juma na Musoma

PENZI limekolea na kinachoonekana sasa kwa Ostaz Juma Namusoma ni kukazia penzi lake kwa mwanadada Blandina Chagula ‘Johari’ anayesumbua kwenye Bongo movies.

 

Kwa mujibu wa mtandao wa GPL zinasema kwamba Ostaz alifunga safari kwenda nchini Afrika Kusini kwa mapumziko mafupi lakini pia kumnunulia mpenzi wake huyo zawadi mbalimbali kwa lengo la kupalilia uchumba wao.

“Jamaa alikuwa Sauzi (Afika Kusini), aliondoka hapa tarehe 17 (Machi) na amerudi tarehe 21. Kamletea zawadi kibao lakini kubwa zaidi ni kamera kubwa, nzuri ya kisasa kwa ajili ya kerekodia filamu,” kilipasha chanzo hicho.

GPL ilifanikiwa kumpata Ostaz kwa njia ya simu, akafafanua: “Ni kweli nilikuwa Afrika Kusini. Kuhusu Johari, ni kweli si mke wangu? Nimemletea zawadi nyingi sana, achana na hiyo kamera unayosema.

“Lengo ni kuweka uchumba wangu  na yeye sawa. Nilitamani sana kusafiri naye lakini sikutaka kufanya hivyo ili kuweka usawa, mke wangu asione nimeegemea zaidi kwa mke mdogo.”

Alipoulizwa kwa nini amemuita Johari mkewe, haraka alisema: “Ndoa ipo karibu, nimeshaamua Johari awe mke wangu wa pili. Wadau wasubiri waone, uzuri ni kwamba dini yangu si kikwazo.”

CREDIT: BONGO MOVIES

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more