SIRI WEMA KUUTOSA MSIBA WA MASOGANGE YAFICHUKA!

BAADA ya kuwa gumzo msibani wakati wa kuagwa kwa mwili wa aliyekuwa video queen kwenye nyimbo mbalimbali za Bongo Fleva, Agness Gerald ‘Masogange’ kutokana na kutoonekana, siri imefichuka ya msanii wa filamu, Wema Sepetu kuutosa msiba huo.

Awali habari zilidai kwamba Wema alishindwa kuhudhuria kwenye msiba huo kutokana na kwamba yeye na marehemu Masogange walikuwa na bifu kali na hawakuwahi kupatana.

“Unajua Wema na Masogange walikuwa hawaivi, sasa inawezekana ndiyo maana hajaonekana msibani. Au ana sababu nyingine? Mimi kwa kweli nimeshangaa kutomuona,” alisikika akisema mmoja wa waombolezaji aliyekuwa amefika katika Viwanja vya Leaders jijini Dar kuuaga mwili wa Masogange.

SIRI YAFICHUKA

Kutokana na gumzo la Wema kuutosa msiba huo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta kwa njia ya simu yake ya mkononi lakini iliita bila kupokelewa. Baada ya kutopokelewa, gazeti hili liliamua kumtafuta meneja wake, Neema Ndepanya ambaye alitoa siri ya Wema kutohudhuria msibani hapo ambapo alisema mwanadada huyo alipatwa na tumbo la ghafla ambalo lilimzuia kutoka kwenda popote.