Mkurugenzi wa Twaleeb Entatainment yenye makazi yake Denmark bado ameendelea kuwasihi wasanii wanaofanya filamu za kiswahili waungane na kuwa kitu kimoja , kwani wote lengo lao ni moja kuutangaza Uafrika , hakuishia hapo , na kusisistiza kama kuna tofauti basi amewaomba viongozi wote wazike tofauti hizo na kuungana ili kuweza kufanya kazi kwa nguvu moja Soma chini alichokisema.
Abou Hermis Twaleb akiwa kwenye pozi mbalimbali
”Ninawaomba wasanii wote mnaofanya MOVIE ZA KISWAHILI mnaoishi EUROPE, Tujumuike na kutengeneza hata FILAM MOJA YA USHIRIKIANO WA VIKUNDI VYOTE, nikimaanisha Twaleb Entertainment, JDP production ,Big JJ ; Mausa Stars Pro , Umoja Stars Pro, V .A.D , N.G.G, T.A.O, na vikundi vingine NORWAY, SWEDEN na kokote kwengine (na hata vikundi ambavyo sikuvitaja hapa ) …ili tuonyesha mshikamano wetu na kuweka kando tofauti zetu, mila zetu, rangi zetu, utamaduni wetu, na hata tabia na tofauti zetu kibinafsi….hii ni kuonyesha mshikamano na kusahau matatizo yetu, tofauti zetu, kutokuelewala kwetu, na pia kuonyesha kuwa ni kitendo cha kusawazisha pale palipokuwa na TATIZO…..Haya ni mawazo yangu tu, kwa kuwa nawapenda wote…na tena nitazidi kuwapenda daima.”
kwa kuwa nawapenda wote..
.Tuamke na kutizama mbele na kusahau tofauti zetu…walionachuki – wasameheane, waliona-kitu au dukuduku moyoni wakutane, waongee wana wasameheane ili tudumishe upendo kati yetu….nini faida ya kuwa mbali-mbali kikazi ?kutofanya kazi pamoja ? kutokutana hata kuzungumzia u-Africa wetu in Europe….hakuna kitakachotupa raha maishani kama kukutana na kucheka, kufurahi, ubadilishana mawazo na kufanya kaz i pamoja…HICHO NDIO KILIO CHANGU NA NITAENDELEA KULIA…….hadi hali itakapokuwa shwari.. .PEACE & LOVE IS WHAT WE NEED …NOW……
Bonyeza hapa kuangalia trailer ya filamu ya kwanza ya kampuni ya TE
Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more
CREDIT : Swahili Talk Radio
Tupe maoni yako hapo Chini..!!