Mwenyekiti wa UTU Mfundo Peter Mfundo Berlin, Ujerumani
Msanii maarufu nchini Tanzania Kutoka kundi la Orijino Komedi al maarufu kama Mpoki (a k a Muarabu wa Dubai) anatarajiwa kuondoka nchini mapema mwanzo wa wiki hii kuenda nchini Ujerumani kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano mkuu wa Umoja wa Watanzania Ujerumani (U T U), utakaoambatana na Kongamano la kibiashara pamoja na Sherehe za Muungano wa Tanzania , zitakazoanza siku ya ijumaa tarehe 25.04.14 na kumalizika siku ya Jumamosi Tarehe 26.04.14. kuanzia saa 7 mchana katika ukumbi wa Deutsche Bank, Unter den Linden 13-15, 10117 Berlin, Ujerumani.
Akiongea na vyanzo vyetu vya habari msanii huyo alisema kuna umuhimu mkubwa wa safari yake ni kuwakilisha wasanii wa Tanzania katika Tamasha hili kubwa la aina yake, aidha aliendelea kufafanua kuwa wakati umefika kwa wasanii wa Tanzania kushirikiana kikamilifu na Watanzania wanaoishi nje ya nchi ili kuweza kupata fursa mbali mbali zilizopo nje ya Tanzania, aliendelea kwa kusema amevutiwa sana na Umoja Wa Watanzania Ujerumani (U T U) kwa shughuli zake mbali mbali ambazo umekwishazifanya nchini humo na ameamua kutoa mchango wake wa hali na mali kuhakikisha (U T U) inafanya vizuri zaidi katika shughuli zake mbali mbali. Ameongeza kwamba yeye binafsi amekuwa ni mfuatiliaji wa karibu sana wa shughuli za umoja huo.
Akiongea na vyanzo vyetu vya habari Mwenyekiti wa Umoja Wa Watanzania Ujerumani U T U Bw. Mfundo Peter Mfundo alithibitisha kwa safari ya msanii huyo Maarufu nchini Tanzania. Alisema U T U Ilipendelea sana wasanii zaidi kuhudhuria sherehe hizi lakini kwa bahati mbaya haikuwezekana kutokana na mambo yalio nje ya uwezo wa U T U, aidha U T U ni chombo kinachokubali sana na kuzifagilia kazi za wasanii wa Tanzania.
Mwenyekiti wa umoja huo anawaalika watanzania wote na waafrika katika sherehe hizo bila kukosa