KUTANA NA MSANII MAARUFU WA FILAMU KUTOKA V.A.D DENMARK , SELEMBE TOKO ANAELIA USANII NI VITA KUBWA .
JINA LAKO HALISI NI NANI NA UNATOKEA WAPI
Jina langu ni selembe toko natokea congo bukabu.
JE UMEOA AU UNA MCHUMBA
hapana sijaoa wala mchumba
ILIKUAJE UKAINGIA KWENYE MOVIE
ilikuwa ni ndoto yangu ya mda mrefu
NI MOVIE NGAPI UMECHEZA MPAKA SASA
Nimeshacheza movie saba , Moyo wangu , Twinsister , Mistreated girl , Jealous Friend , Tanzania to Denmark na lucy Komba na nyingine mbili bado hazijatoka
MPAKA KUFIKIA HAPO KISANII UNGEPENDA KUMSHUKURU NANI
Kwanza kabisa ningependa kumshukuru mungu alienipa uhai na nguvu ,pili ningependa kumshukuru LUCY KOMBA kwa kugundua uwezo wangu na kucheza nae movie yake ya Tanzania to Denmark iliyosababisha nipate mashabiki wengii ulaya na africa
KWA NINI UNASEMA USANII NI VITA
Unajua unapokuwa msanii tu unakuwa tayari kama kioo cha jamii, na kama msaanii wapo watakaokupenda na wapo watakaokuchukia hapo sasa ndio matatizo yanapoanza wataanza kusema ooh umechukua mke wangu ooh una roho mbaya ili mradi tu wakushushe , na wakati mwingine unaweza kupata kazi mtu anatka afanye na selembe lakini kutokana na wivu na chuki binafsi basi mtu anasema kama fulani yupo hatuwezi kushuti mcancel huyu
WEWE UNA UGOMVI NA MSANII AU MTU YOYOTE
samahani nisingependa kuendelea kuongelea hilo nitakapokuwa tayari ntaongea waziwazi ila kwa sasa niko kikazi zaidi , kwani nina mengi ya kusema ila naomba niishie hapo ila hii kazi ni kazi ya vita sana.
JE UNA LOLOTE UNGEPENDA KUWAAMBIA MASHABIKI WAKO NA MIPANGO YAKO YA BAADAE KWENYE EUROPE MOVIE INDUSTRY
Nawapenda sana mashabiki wangu wote waliopo ulaya america na africa ila mniunge mkono kwenye kazi zangu na nina mpango wa kwenda africa kufanya kazi na wasanii mbalimbali ili niwape mashabiki wangu radha mbalimbali ila waniombee kwani usanii ni vita
hahahha swahili movie inakushukuru sana Mr selembe toko kwa ushirikiano uliotoa kuanzia mwanzo mpaka mwisho , kama unaswali au maoni usisite kuacha coment zako au kututafuta kwa facebook page yetu swahili movies .com ……